First blog post

This is your very first post. Click the Edit link to modify or delete it, or start a new post. If you like, use this post to tell readers why you started this blog and what you plan to do with it.

post

Advertisements

SPIKA AKATAA TRUMP KUHUTUBIA BUNGE-uingereza.

Spika wa bunge la Uingereza John Bercow

Spika wa Bunge la Uingereza John Boscow amekosolewa kwa kupinga hatua ya rais Donald Trump kuhutubia bunge la taifa hilo wakati wa ziara yake.

Mwanachama wa chama cha kihafidhina aliambia BBC kwamba matamshi yake yamesababisha chuki huku mbunge mmoja akisema kuwa hayafai huku wengine wakidai hafai kupendelea upande mmoja.

Bw Bercow alisema pingamizi dhidi ya ”ubaguzi wa rangi na ule wa kijinsia” zinapaswa kuangaziwa sana na wanachama wa bunge hilo.

Mbunge wa Marekani Joe Wilson alisema kuwa ni pigo kwa chama cha Trump cha Republican.

Mwandishi wa BBC wa maswala ya kisiasa Eleanor Garnier amesema kuwa ni pigo la kidiplomasia kwamba rais Trump hataruhusiwa kuhutubia bunge la nchi hiyo.

Mwezi uliopita waziri mkuu wa Uingereza Theresa May alisema kuwa rais Trump amekubali mwaliko kutoka kwa malkia wa Uingereza kwa ziara rasmi nchini Uingereza baadaye mwaka huu.

Lakini akizungumza bungeni siku ya Jumatatu bw Bercow alisema kuwa anapinga rais Trump kuhutubia mabunge yote kama ilivyo ada na viongozi wengine wa kimataifa.

Amesema kulihutubia bunge sio haki bali ni heshima anayopewa kiongozi wa kimataifa.

:source BBC

VIONGOZI WA MIKOA MINGINE NA NYIE IBUENI MATATIZO NDANI YA MAENEO YENU ACHENI KWENDA NA UPEPO WA MAKONDA.

Dar es salaam ni moja ya majiji ambayo yanakua kwa kasi na kama wengi wanavyoliita kwa sasa kama jiji la Makonda limeendelea kuteka vichwa vya habari ndani na nje ya Tanzania kutokana na habari zinazotoka ndani ya jiji hili.

Na hii inatokana na wengi wa watu maarufu kuishi ndani ya jiji hili lakini pia maamuzi ya viongozi ndani ya jiji hili.Ni siku chache tu toka Mkuu wa mkoa huo kutangaza rasmi kuanza kupambana na madawa ya kulevya na kuapa kula nao sahani moja wahusika wote ili kuhakikisha tatizo hilo  linatokomea ndani ya mkoa wake.

Related image

Lakini cha ajabu ni kuwa baadhi ya viongozi wengi kwenye mikoa mingine wamekua wakienda kwa upepo wa jiji hili la makonda pasipo kua na future yao kama mkoa ili kushughulika na matatizo yanayoikumba jamii wanayo iongoza.

Sisemi kuiga ni jambo baya lakini tujiulize wote kwa nini mpaka jiji la Makonda liamue kwanza ndo tuone mikoa mingine ikifata nyayo ni kweli hakuna matatizo ambayo wakuu wa mikoa mingine hawawezi kuibua na kuisaidia jamii au ni kwa sababu fikra nazo chache ?? au woga kwa sababu ya kutojiamini kwa wanalolifanya??

Ni vema kila kiongozi akawajibika ipasavyo katika sehemu anayo iongoza kwa kusimamia yale anayoyaamini na si kufata upepo wa majiji ya watu, tusisubiri jiji la Dar es salaam liamue ndo na sisi tuanze kufanya lazima Tuanze sisi na wao waige.

mkonoupdates.

Mwanafunzi wa mbeya leo amekamatwa na kete 24 za cocaine katika eneo la Mbalizi jijini Mbeya.

Image result for cocaine

Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya akizungumza amesema polisi wamemkamata akiwa akiziuza kwa watu mbalimbali na ameongeza kua uchunguzi bado unaendelea ili kuwakamata mapapa wa biashara hiyo haramu.

Pia amesema kua vita hiyo ilikua ikiendelea lakini kwa sasa imepewa Nguvu ili kuweza kuliondoa kabisa.

posted by

mkonoupdates.

MANENO 83 YA ZITTO KABWE KUHUSU SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA LINALO ENDELEA DAR ES SALAAM.

 

Related image

“Kamati (ya Bunge) imelalamika kuwa Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya ina bajeti finyu na hata hiyo bajeti haitolewi na hivyo kusababisha Mamlaka kukosa vitendea kazi, kushindwa kutoa elimu kwa umma, kushindwa kufanya operesheni za ukamataji wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya na kushindwa kutoa ushauri nasaha kwa waathirika,” alisema Zitto

Baadhi ya watuhumiwa wameelezwa kuteswa na kupigwa na polisi na kulazimishwa kutoa maelezo kwa Polisi,” alisema Zitto. “Umma haujaelezwa kama watu hawa wamekamatwa na madawa hayo ama wamehisiwa kuwa ni watumiaji tu.

ZITTO AUNGANA NA WABUNGE WENZAKE KUPINGA KUKAMATWA KWA LISU.

Wabunge wote wa vyama vya upinzani waliokuwa bungeni katika kikao kinachoendelea jioni hii wametoka nje ya Bunge, wakipinga wenzao kufukuzwa bungeni pamoja na kitendo cha Mbunge Tundu Lissu kukamatwa.
Wabunge waliokuwa wameamuliwa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge na Naibu Spika Dkt Tulia Ackson ni pamoja na mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya na Mbunge wa Serengeti Marwa Ryoba.
Wabunge hao watatu wamedaiwa kupinga uamuzi wa Naibu Spika kuhusu muongozo ulioombwa na mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, kuhusu utaratibu uliotumika kumkamata mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Mara baada ya Naibu Spika kutoa maamuzi ya kuwaondoa wabunge hao watatu bungeni, ndipo wabunge wengine wa upinzani pia wakaamua kutoka kama ishara ya kupinga maamuzi hayo, pia ikiwa ni ishara ya kupinga utaratibu wa kukamatwa kwa mbunge Tundu Lissu.
Nje ya ukumbi wa Bunge, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe , amesema wamefikia hatua hiyo kuonesha kuwa uataratibu unaotumiwa kukamata wabunge wakiwa bungeni siyo sahihi, na kwamba kesho wataendelea na vikao vya bunge lakini mapambano yataendelea.
“Kesho tunarudi bungeni, lakini mapambano yataendelea, tunataka kuonesha kuwa utaratibu huu wa kuvizia wabunge kwenye milango ya bunge bila taarifa rasmi ya Spika na bila kuwaeleza wabunge sababu za kukamatwa kwao siyo sawa. Tukilifumbia macho litakuja kumtokea mbunge yoyote hata wa CCM” Amesema Zitto.