BODI YA MIKOPO YAANZA KUPOKEA MAREJESHO YA WADAIWA SUGU.

Bodi ya mikopo ya elimu ya juu baada ya kutangaza majina ya wadaiwa sugu na kutishia kutangaza majina yao kwenye vyombo vya habari  na kuyachapisha kwenye magazeti hatimaye wadaiwa hao sugu kwa mujibu wa bodi waanza kulejesha.

5

Akizungumza na Gazeti la Habari Leo kwa njia ya simu Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru, alisema kwa sasa mwitikio wa wanufaika kuanza kulipa madeni yao ni mkubwa ikilinganishwa na siku za nyuma.

“Ukweli ni kwamba, mwitikio ni mkubwa, wengi wanajitokeza kulipa, wiki iliyopita tulikuwa na idadi ya wanufaika takribani 42,000 waliokuja kulipa lakini hadi leo (jana) wameongezeka na kufikia 45,000 na wanaendelea kuongezeka,” alisisitiza Badru.

posted:frank

at 11:03 am

Advertisements