HUNA KUANZIA LAKI MOJA CHIBU PERFUME HUPATI.

chibuperfume-diamond-platnumz

mashabiki wa Diamond platnumz walipatwa na shauku  kubwa pale msanii huyo alipoitambulisha perfume yake mpya iitwayo “chibu perfume” mwaka jana 2016 kupitia mtandao wake wa instagram na kuahidi kuwa sokoni mda wowote ule.

Ijumaa hii meneja wa msanii huyo, kupitia ‘Insta Live’ amedai tayari mzigo wa perfume hizo umeshaingia mjini na utapatikana katika maduka mbalimbali nchini.

“Mzingo umeingia, utapatikana kila sehemu bado hatujapanga bei,” alisema Sallam huku akionyesha perfume hizo.

Meneja huyo alidai perfume hizo hazitapatikana kwa bei ya chini ya laki moja na huwenda bei ikaongezeka kutokana na ubora manukato hayo.

 

Advertisements