MUIGIZAJI WA GOING BONGO MTANZANIA ERNEST NAPOLEON ACHAGULIWA KUSIMAMIA kampuni ya kimataifa ya utengenezaji na usambazaji filamu

Image result for going bongo ernet napoli

Ikiwa na makao makuu yake jijini New York na ofisi mjini Berlin, Cape Town na Buenos Aires, Napoleon atakuwa na cheo cha pili kwa ukubwa baada ya CEO, Dexter Davis kwenye kampuni hiyo.

Napoleon atasimamia zaidi kazi za kampuni hiyo upande wa Afrika na Mashariki ya Kati, japo hiyo haimaanishi kuwa hatohusika na masuala mengine ya kampuni hiyo duniani kote.

“Hii ni fursa ya kipekee katika hatua hii ya career yangu. D Street Media Group ni kampuni ya kujitegemea inayokua kwa kasi ikiwa imeshika kila upande wa dunia. Ni heshima kubwa kwangu kuendeleza biashara yetu katika masoko ya Afrika na Mashariki ya Kati ambayo nayaelewa vyema,” amesema Napoleon.

Aliendelea, “Naamini kuna fursa nyingi kwa kampuni ya Kimarekani kama D Street barani Afrika, na tukiwa na washirika sahihi kutengeneza maudhui mazuri, tutafanikiwa Afrika na hasa Marekani na nje ya nchi.”

Kwa upande wake, Davis alisema, “Ninafurahi kuleta mshirika mchangamfu kama Ernest, sifa zake kama muigizaji na mtayarishaji, kutamfanya awe rais mzuri. Kwa haraka amekuwa na jina Tanzania, sehemu aliyozaliwa baba yake na ambako amekulia. Nimesikia mambo ya kuvutia kuhusu Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, na ninafurahi kuwa na Ernest ndani yetu kutuongoza katika mafanikio ndani ya bara la Afrika,” alisema Davis.

“Kuhusu ukweli kuwa Ernest anazungumza Kiswahili, Kirusi, Kiswidishi na Kiingereza, ni asset pia. Ongeza hapo ukweli kuwa ni mtayarishaji anayetaka kuileta Afrika na Waafrika kwenye jukwaa la dunia ni kitu ambacho kimenifurahisha na kujivunia zaidi.”

D Street tayari ina uwepo wake barani Afrika ikiwa na ofisi Cape Town, Afrika Kusini. D Street Pictures, tawi la utayarishaji, lilitayarisha filamu ya Afrika Kusini, iitwayo ‘Musiek vir die Agtergrond,’ filamu ya Kiafrikaan iliyowekeza mwaka 2013.

Kampuni sasa ipo kwenye utayarishaji wa mwanzo wa filamu iitwayo ‘The Blue Mauritius.’ Muingozaji wa Uingereza, Charles Henri Belleville, (Jet Trash, The Inheritance) ataiongoza. Belleville amemaliza kuongoza filamu yake ya pili na mtajwa wa tuzo za Oscar, Tom Hardy (Mad Max, Legend).

Kisa cha filamu ya ‘The Blue Mauritius’ kinawahusu wezi watano wa kimataifa wanaoenda Cape Town kuiba muhuri wenye thamani zaidi duniani. Filamu hiyo imekusanya mastaa duniani akiwemo muigizaji wa Marekani, Eric Dane (Grey’s Anatomy, Last Ship), Brian Cox (The Rise of the Planet of the Apes, The Bourne Supremacy), John Ryes-Davies (The Lord of the Rings, Raiders of the Lost Ark) nguli wa Ufaransa, Gerard Depardieu (Life of Pi, The Man in the Iron Mask), kutaja wachache tu.

Advertisements