TUNAITAJI KUFANYA HAYA SHULE ZA SELIKALI KUONGOZA KITAIFA.

 

Ukitazama kwenye chati hapo juu utaona jinsi gani shule binafsi zilivo tamba matokeo kidato cha nne kwa mwaka 2016 na hii ni ishara kwamba shule nyingi za private zimejipanga kuendelea kuzinyanyasa shule za serikali ambazo wengi wanaziita SAINT KAYUMBA.

Miaka ya nyuma shule kama IHUNGO,KIBAHA,PUGU,TABORA BOYS na TABORA GIRLS zilionekana kufanya vizuri matokeo ya kidato cha nne lakini mwaka huu hakuna hata moja iliyoingia kumi bora.Wito kwa selikali ni kuendelea kuhakikisha shule zote za selikaliĀ  Tanzania kwanza zinapata walimu wakutosha lakini pia kuangalia upya namna walimu wanavyo andaliwa vyuoni kwa kuweka miundo mbinu rafiki kwao ili kuwawezesha kupata ujuzi wa kutosha ili na wao wakawapatie wanafunzi.

Mwisho kabisa selikali imekuwa ikiandaa walimu mbalimbali lakini changamoto inakuja pale shule binafsi zinapo wachukua na kuwalipa misharaha mizuri hivyo kusababisha kufundisha kwa kujituma na kwa weredi wa hali ya juu ivyo basi selikali ihakikishe wale walimu bora inaowaanda kwenye vyuo mbalimbali nchini inawatunza kwa kuwaandalia mazingira mazuri ya utendaji kazi lakini pia kwa kuwalipa vizuri kama shule za binafsi zinavofanya.

Kwa kufanya hivyo ni hakika ufaulu wa shule za selikali utapanda na tutaanza kuziaona kumi bora zikitawala zaidi ya hivi tunavyoona sasa.

posted

by

mkonoupdates.

 

Advertisements