PICHA:Cameroon bingwa AFCON 2017.

 

 

Advertisements

YANGA KUWAKABILI WACOMORO-Ligi ya mabingwa Afrika.

Image result for MASHABIKI YANGA

Klabu ya soka ya Yanga inatarajiwa kuondoka Ijumaa ijayo kwenda Comoro kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Ngaya Club.

Huu ni msimu wa pili mfululizo kwa klabu ya Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na inaanza na timu za Comoro baada ya mwaka jana pia kuitoa Cercle de Joachim kwa jumla ya mabao 3-0, ikishinda 1-0 ugenini na 2-0 nyumbani katika Raundi ya Awali.

Katika Raundi ya Kwanza Yanga iliitoa APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda 2-1 ugenini na kutoa sare ya 1-1 nyumbani.

Mbio za Yanga katika Ligi ya Mabingwa ziliishia Raundi ya Pili inayohusisha timu 16, baada ya kutolewa na wababe wao wa kihistoria, Al Ahly ya Misri kwa jumla ya mabao 3-2, ikitoa sare ya 1-1 Dar es Salaam kabla ya kwenda kufungwa 2-1 Alexandria ndani ya dakika 120 baada ya mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.

Yanga ikaangukia katika kinyanga’anyiro cha kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako iliitoa Sagrada Esperanca ya Angola kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 2-0 Dar es Salaam Mei 7 na kufungwa 1-0 Mei 18 katika mchezo wa marudiano Esperanca, Angola.

Katika mechi za makundi, Yanga ilishinda mchezo mmoja tu dhidi ya MO Bejaia ya Algeria Agosti 13, 2016 na kutoa sare moja na Medeama ya Ghana Julai 16, 2016 zote uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi nyingine ilifungwa 1-0 Bejaia Juni 20 ugenini, ikafungwa 1-0 nyumbani na TP Mazembe ya DRC Juni 28, ikafungwa 3-1 na Medeama Julai 26 ugenini kabla ya kumaliza kwakipigo cha 3-1 mbele ya Mazembe Agosti 23 mwaka jana Lubumbashi.

Uingereza kuondolewa Fainali kombe la dunia 2018-FIFA.

Shiikisho la soka duniani FIFA

Hofu imeanza kutanda kwa mashabiki wa soka nchini humo jambo hili linaweza kuwatoa Uingereza katika michuano ijayo ya kombe la dunia nchini Russia ,Endapo bunge litapiga kura wiki ijayo basi itaiweka Uingereza katika hali ya sintofahamu juu ya ushiriki wao katika kombe la dunia la mwaka 2018.

Mgogoro kati ya bunge la Uingereza na FA unakuja baada ya baadhi ya viongozi wa zamani wa FA kudai kwamba chama hicho kinashindwa kujiendesha.Katika barua ambayo viongozinwa zamani wa FA walimuandikia mwenyekiti wa kamati ya michezo bungeni bwana Damians Collin inaelezwa kwamba FA imekwama na imeshindwa kujiendesha.Inasubiriwa kwa hamu kuona nini kitatokea baada ya kikao cha bunge la Uingereza kutoa maamuzi yao kuhusu FA.

Kesi hii ya Uingereza haina utofauti na kesi iliyokuwa ikiwakabili Kuwait katika hatua ya kushiriki kombe la dunia 2018.Serikali ya Kuwait iliingilia masuala ya soka nchini humo.Wakiwa wamefika raundi ya tatu ya mechi za kufuzu kombe la dunia FIFA waliamua kuwatoa Kuwait katika mashindano hayo baada ya serikali yao kukiuka sheria za Fifa.

Uingereza ambao hadi sasa wako katika nafasi nzuri ya kufuzu kombe la dunia kwani wanaongoza kundi lao la F. Uingereza wamebakiza mechi 6 tu kufuzu kombe la dunia lakini sheria za FIFA zinaweza kuwazuia kufuzu ama kuendelea na mechi zao kwa sasa

Source BBC

mkonoupdates.