VIONGOZI WA MIKOA MINGINE NA NYIE IBUENI MATATIZO NDANI YA MAENEO YENU ACHENI KWENDA NA UPEPO WA MAKONDA.

Dar es salaam ni moja ya majiji ambayo yanakua kwa kasi na kama wengi wanavyoliita kwa sasa kama jiji la Makonda limeendelea kuteka vichwa vya habari ndani na nje ya Tanzania kutokana na habari zinazotoka ndani ya jiji hili.

Na hii inatokana na wengi wa watu maarufu kuishi ndani ya jiji hili lakini pia maamuzi ya viongozi ndani ya jiji hili.Ni siku chache tu toka Mkuu wa mkoa huo kutangaza rasmi kuanza kupambana na madawa ya kulevya na kuapa kula nao sahani moja wahusika wote ili kuhakikisha tatizo hilo  linatokomea ndani ya mkoa wake.

Related image

Lakini cha ajabu ni kuwa baadhi ya viongozi wengi kwenye mikoa mingine wamekua wakienda kwa upepo wa jiji hili la makonda pasipo kua na future yao kama mkoa ili kushughulika na matatizo yanayoikumba jamii wanayo iongoza.

Sisemi kuiga ni jambo baya lakini tujiulize wote kwa nini mpaka jiji la Makonda liamue kwanza ndo tuone mikoa mingine ikifata nyayo ni kweli hakuna matatizo ambayo wakuu wa mikoa mingine hawawezi kuibua na kuisaidia jamii au ni kwa sababu fikra nazo chache ?? au woga kwa sababu ya kutojiamini kwa wanalolifanya??

Ni vema kila kiongozi akawajibika ipasavyo katika sehemu anayo iongoza kwa kusimamia yale anayoyaamini na si kufata upepo wa majiji ya watu, tusisubiri jiji la Dar es salaam liamue ndo na sisi tuanze kufanya lazima Tuanze sisi na wao waige.

mkonoupdates.

Advertisements

TUNAITAJI KUFANYA HAYA SHULE ZA SELIKALI KUONGOZA KITAIFA.

 

Ukitazama kwenye chati hapo juu utaona jinsi gani shule binafsi zilivo tamba matokeo kidato cha nne kwa mwaka 2016 na hii ni ishara kwamba shule nyingi za private zimejipanga kuendelea kuzinyanyasa shule za serikali ambazo wengi wanaziita SAINT KAYUMBA.

Miaka ya nyuma shule kama IHUNGO,KIBAHA,PUGU,TABORA BOYS na TABORA GIRLS zilionekana kufanya vizuri matokeo ya kidato cha nne lakini mwaka huu hakuna hata moja iliyoingia kumi bora.Wito kwa selikali ni kuendelea kuhakikisha shule zote za selikali  Tanzania kwanza zinapata walimu wakutosha lakini pia kuangalia upya namna walimu wanavyo andaliwa vyuoni kwa kuweka miundo mbinu rafiki kwao ili kuwawezesha kupata ujuzi wa kutosha ili na wao wakawapatie wanafunzi.

Mwisho kabisa selikali imekuwa ikiandaa walimu mbalimbali lakini changamoto inakuja pale shule binafsi zinapo wachukua na kuwalipa misharaha mizuri hivyo kusababisha kufundisha kwa kujituma na kwa weredi wa hali ya juu ivyo basi selikali ihakikishe wale walimu bora inaowaanda kwenye vyuo mbalimbali nchini inawatunza kwa kuwaandalia mazingira mazuri ya utendaji kazi lakini pia kwa kuwalipa vizuri kama shule za binafsi zinavofanya.

Kwa kufanya hivyo ni hakika ufaulu wa shule za selikali utapanda na tutaanza kuziaona kumi bora zikitawala zaidi ya hivi tunavyoona sasa.

posted

by

mkonoupdates.