MANENO 83 YA ZITTO KABWE KUHUSU SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA LINALO ENDELEA DAR ES SALAAM.

 

Related image

“Kamati (ya Bunge) imelalamika kuwa Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya ina bajeti finyu na hata hiyo bajeti haitolewi na hivyo kusababisha Mamlaka kukosa vitendea kazi, kushindwa kutoa elimu kwa umma, kushindwa kufanya operesheni za ukamataji wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya na kushindwa kutoa ushauri nasaha kwa waathirika,” alisema Zitto

Baadhi ya watuhumiwa wameelezwa kuteswa na kupigwa na polisi na kulazimishwa kutoa maelezo kwa Polisi,” alisema Zitto. “Umma haujaelezwa kama watu hawa wamekamatwa na madawa hayo ama wamehisiwa kuwa ni watumiaji tu.
Advertisements

TRUMP AMULAUMU JAJI NA MFUMO WOTE WA MAHAKAMA.

Mapema mahakama ya rufaa ilikataa ombi la serikali ya Marekani la kurejesha amri ya marufuku ya kuwazuia wahamiaji ambapo ofisi ya mwanasheria mkuu imepewa hadi leo Jumatatu kujibu maamuzi hayo.

Image result for TRUMP

Rais Donald Trump amewaagiza maafisa wa usalama wa mipakani kuwakagua kwa makini watu wanaoingia Marekani ,huku marufuku yake dhidi ya raia wa mataifa 7 ya kiislamu ikiwa imesimamishwa.

Amesema kuwa iwapo kutakuwa na tukio lolote jaji huyo na mfumo wote wa mahakama utalaumiwa.

Japanese Prime Minister Shinzo Abe prepares for serious match with Trump

TOKYO — Japanese Prime Minister Shinzo Abe will meet U.S. President Donald Trump this weekend amid concern that results of the meeting may greatly affect the Japanese economy.

The first Japan-U.S. summit since Trump took office will be held in Washington on Friday and at the new U.S. leader’s estate in Palm Beach, Florida, on Saturday. The two may play golf at the Trump estate to deepen their friendship.

The meeting will be a “more serious match than ever,” a senior Japanese government official said, as the Trump administration has yet to be fully staffed, preventing the usual preparations before national leaders meet on the details of issues on the agenda. Trump should “make light of” Abe if the Japanese side takes the stance that it will “bring home the president’s demands for study,” the official added.

Abe will be accompanied by Finance Minister Taro Aso, Foreign Minister Fumio Kishida and Economy, Trade and Industry Minister Hiroshige Seko. The exchange of heated arguments between the two leaders is expected.

Trump has repeatedly slammed Japan on trade with the U.S. and the yen-dollar exchange rate. Although it is uncertain what Trump will bring to the table, bilateral trade, especially Japan’s automobile imports and exports, is the matter of greatest concern on the Japanese side.

Trump has consistently stressed the need for creating jobs in the U.S. and narrowing the country’s trade deficit while targeting companies that export to the U.S. He has specifically called out Toyota Motor and other Japanese automakers.

“I will explain Japanese companies’ contribution to the U.S. economy and dispel the president’s misunderstanding,” Abe said, noting that increased production at Japanese automakers’ plants in the U.S. has “already created 1.5 million jobs.”

It is likely that the two sides will discuss a bilateral trade deal as well.

source Asian review.

MO DEWJI APATA PIGO APEWA NOTISI YA SIKU 14 NA MAOFISA ARDHI.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza oparesheni maalumu ya kukusanya Kodi ya Pango la Ardhi kutoka kwa wadaiwa sugu wa Makampuni, mashirika ya kiserikali na watu binafsi kwa kuwafuata katika maeneo yao.

Katika hatua ya kwanza Wizara kwa kushirikiana na Manispaa za  mkoa wa Dar es salaam imetoa notisi kwa wadaiwa sugu wa kodi ya pango la Ardhi wakiwemo Mohammed Enterprises anaedaiwa Shilingi milioni 73, Lamada  Hotel anaedaiwa Shilingi milioni 54, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) anaedaiwa Shilingi milioni 144 na Tanganyika Motors anaedaiwa Shilingi milioni 22.

 

Makampuni hayo yamepewa notisi ya siku 14 ili kulipa kodi hizo wanazodaiwa na endapo hawatalipa watafutiwa umiliki au mali zao kwa kupigwa mnada ili kufidia gharama wanazo daiwa.
Serikali kwa kutumia kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment imeendesha oparesheni hiyo kwa kufika katika ofisi za wamiliki wa viwanja na mashamba makubwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Akiongea kwa kusisitiza, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila amesema katika mwaka wa fedha 2016/17 Wizara imepanga kukusanya Sh. bilioni 111.77 kutokana na Kodi ya Pango la Ardhi.
Wizara haitaweza kufanikisha malengo hayo endapo itaendelea kuwaachia wadaiwa sugu ambao hawataki kulipa kodi. Kwani kwa miaka mingi sasa mapato mengi ya serikali yamekuwa yakiachwa kutokana na kushindwa kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi Kayandabila alisisitiza.
Wafanyakazi wa Lamada Hotel (kushoto) wakiangalia kwa makini Notisi ya madai ya kodi ya Ardhi wakati ikiwasilishwa na watumishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akiongea na waandishi wa habari kwamba Serikali kupitia Wizara yake haitamuacha mtu au kampuni yoyote inayodaiwa kodi ya Ardhi hata kama ni Taasisi ya serikali.
BY
mkonoupdates.

SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA NA WASANII DAR ES SALAAM BUSARA ITUMIKE-NAPE.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye ameingilia kati na kutaka busara itumike katika zoezi la kutaja wasanii wanaohusika na dawa za kulevya linalofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

 

Nape ametoa ushauri huo leo Mjini Dodoma wakati akizungumza na wanahabari kuhusu sheria mpya wa huduma za habari, ikiwa ni siku nne tangu mkuu huyo wa mkoa aanze kutaja wahusika wa dawa za kulevya wakiwemo wasanii wa bongo fleva na filamu.
Baadhi ya waliotajwa na kutakiwa kuripoti polisi kwa mahojiano ni pamoja na Vanessa Mdee, Wema Sepetu, Nyandu Toz, Chidi Benz, TID, Tunda, Babuu wa Kitaa n.k

 

Nape baada ya kuulizwa swali na wanahabari kuhusu suala hilo amesema kuwa wizara yake inakiri kuwa tatizo hilo ni kubwa, na ilifikia hatua ya kuwasaidia baadhi ya wasanii kwenda kupata matibabu akiwemo msanii Ray C na kwamba wanaunga mkono jitihada zozote za kupambana na tatizo hilo.
Amesema tatizo lipo kwenye namna ya kuwaadhibu wanaogundulika kutumia dawa za kulevya, kwa maana ya sheria ipi itumike kuwashitaki, lakini pia tatizo lingine ni busara inayotumika kuwataja na kuwakamata watu ambao tayari wamekwisha athirika na dawa kulevya badala ya kuwasaidia.
Kwa mtazamo wake nape amesema hilo ni tatizo la jamii nzima, na kushauri jamii yote ya watanzania kushiriki katika kujenga maadili ya watoto.
BY
mkonoupdates.

MZOZO ANGLIKANA WAENDELEA ASKOFU MOKIWA AZUILIWA NA POLISI KAGERA KUSHIRIKI IBADA.

Polisi  wameingilia kati mvutano ndani ya Kanisa la Anglikana baada ya kumzuia Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam, Dkt. Valentino Mokiwa kushiriki ibada ya kumsimika Askofu mpya wa Dayosisi ya Lweru.
Askofu Mokiwa amekuwa katika mvutano na Askofu Mkuu wa Anglikana Tanzania, Dkt. Jacob Chimeledya tangu alipotangaza kumvua  uongozi wa Dayosisi ya Dar es Salaam, akidai mkuu huyo hakufuata utaratibu na kwamba hana mamlaka ya kuchukua uamuzi huo.
Aidha Askofu Mokiwa aliwasili makao makuu ya Dayosisi ya Lweru mjini Muleba mkoani Kagera na alitarajiwa kuungana na maaskofu wengine kumsimika Godfrey Mbelwa kuwa askofu mpya wa dayosisi hiyo.
Lakini taarifa zilizopatikana  zimesema Askofu Mokiwa alichukuliwa na polisi na kuhojiwa katika kituo cha Muleba, kutokana na kuhofu kuwa kuwapo kwake kungeweza kusababisha vurugu katika ibada iliyokuwa iongozwe na Dkt. Chimeledya kutokana na mvutano uliopo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Augustino Ollomi,amesema kuwa jeshi hilo halikumkamata Askofu Mokiwa na kumhoji, badala yake amesema walichukua hatua haraka baada ya kupata taarifa za kiintelijensia kuhusu masuala ya usalama.
“Ni wajibu wetu kufuatilia, tulimuonya kuhusu suala la kuhudhuria ibaada kwa sababu kulikuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani lakini ilikuwa ni hiari yake kutohudhuria, huo utakuwa ni uamuzi wake,” amesema Ollomi.
Kamanda Ollomi amesema walimuita Askofu Mokiwa juzi saa moja usiku kwa ajili ya kumpa ushauri wa kutohudhuria sherehe hizo kwa kuwa mgogoro uliopo katika kanisa hilo ungeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
posted by
mkonoupdates

JOKATE NA WABUNGE VITI MAALUM CCM WAKIWA KWENYE SHAMBA LA ZABIBU WILAYANI CHAMWINO-DODOMA.

Mbunge wa Viti maalum kundi la vijana, Mariam Ditopile Mzuzuri akiwa na vijana wa CCM wakielekea lililopo shamba la Zabibu.

Wakiwa shambani wakikagua shamba hilo.

MBUNGE wa viti maalum Mariam Ditopile Mzuzuri amewasihi vijana kujishughulisha na shughuli za kilimo hususan kilimo cha zabibu ili kujiinua kiuchumi na kuondokana na tatizo la ajira.
Hatua hiyo ni  kuunga mkono na kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya Rais Dk.John Magufuli ya hapa kazi tu na kuwa na Tanzania ya Viwanda.
Mariam alitoa rai hiyo mjini hapa  wakati alipofanya ziara ya kutembelea Shamba la Zabibu la  Chinangali II, akiambatana na vijana wa Chama cha Mapinduzi kwa lengo la kujifunza namna ya uzalishaji, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 ya kuzaliwa kwa CCM.
Alisema imefika wakati warudi na kuitekeleza kauli ya kama unataka mali utaipata shambani, ambayo itafanikiwa kwa watanzania kuwekeza kwenye shughuli za kilimo.
” kimsingi Zabibu ya Dodoma licha ya kutumika kutengeneza mvinyo ambao unasafirishwa ndani na nje ya nchi lakini bado haijatangazwa kiasi cha kutosha na kusababisha soko lake kuwa chini,”alisema Mariam.
Alisema imefika wakati vijana wa CCM kutumia fursa hiyo ikiwa ni pamoja na kuitangaza Zabibu ya Dodoma, na hasa ukizingatia kipindi hiki ambacho nchi inakwenda kuwekeza katika viwanda.
“Mimi kijana mwenzenu nawasihi mtumie vyema fursa hii ili muweze kujikwamua kiichumi, nimetumia nafasi hii kuwaleta ili mje kujifunza namna kilimo cha Zabibu kinavyotekelezwa ili nanyi muweze kuiga mfano huo kwa vitendo,”alisema.
Naye Mbunge wa Viti Maalum, Maria Kangoye aliyeambatana na Mariam katika ziara hiyo, aliisihi  serikali yake sikivu ya CCM kuhakikisha inawawezesha vijana kikamilifu kupitia ile asilimia 5, ambayo ipo kisheria na imekuwa ikitengwa wakati wote.
Pia aliwasihi vijana wa CCM, kuacha kubweteka na badala yake wafanye kazi na kujitokeza kushiriki kikamilifu katika shughuli za kilimo.

Kwa upande wake Jokate Mwogelo ambaye pia aliambatana na mbunge Mariam katika ziara hiyo aliwataka vijana kutotumia muda mwingi katika mitandao ya kijamii kwa kuzungumza mambo yasiyofaa.

“Sisi vijana wa CCM tubadilike, tutumie mitandao hii kujiinua kiuchumi, tuelezane na kupashana habari za fursa zilizopo na hapo tutafanikiwa, alisema Jokate.
Shamba hilo la Zabibu la Chinangali II, hadi kufikia Julai 2016 lilikuwa na jumla ya ekari 295 ambazo zimeendelezwa kwa ruzuku kutoka serikali kuu na halmashauri ya wilaya ya Chamwino na mkopo wa Benki ya CRDB wa jumla ya Sh.bilioni 1.5.

Pia shamba  hilo lenye ukubwa wa ekari 1,250 lilianzishwa mwaka 2008 na  likikusudiwa kutoa mchango mkubwa wa kupunguza umasikini kwa vijana, wanawake na kutoa ajira kwa jamii ya vijiji sita vinavyozunguka eneo la mradi.